Dkt. Tulia akabidhi kadi ya shukrani Hospitali ya Rufaa Mbeya

0
227

Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amekabidhi kadi ya shukrani kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa niaba ya familia ya Baba Askofu Rabbi Mwakanani wa Kanisa la The Evangelical Brotherhood Church.

Dkt. Tulia amekabidhi kadi hiyo ya shukrani katika ibada ya mazishi ya mke wa Askofu Mwakanani katika Kanisa la Uinjilisti la Undugu Ushirika wa Wana wa Mungu, Mbeya Mjini na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt Godlove Mbwanji.

Kadi hiyo ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rhoda Mwakanani (Mke wa Askofu) alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo hadi umauti ulipomkuta Julai 2, 2020.

Tukio hilo limeshuhudiwa na watu mbalimbali akiwemo Baba Askofu Rabbi Mwakanani mwenyewe na Katibu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Myriam Msalale.