Joshua Nassari apokelewa rasmi CCM

0
553

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiunga Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika mkutano wa kupokelewa na viongozi wa CCM Mkoa wa Arusha Nassari amesema kuwa amejiunga chama hicho ili kujiweka katika upande mmoja na wale wanaoitaki nchi hii maendeleo.

Nassari ameongeza kuwa serikali ya Rais John Magufuli imefanya mambo mengi ambayo amekuwa akiyapigania kama vile kuboresha elimu, huduma za afya na ujenzi wa miundombinu pamoja na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati, hivyo hakuna sababu yeyote ya kumpinga.

Mwanasiasa huyo kijana alivuliwa ubunge wake Machi 2019 kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya bunge mfululizo bila ruhusa, kitendo ambacho ni kinyume na sheria.