Wakati maonesho ya Sabasaba yakiendelea jijini Dar es Salaam, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linakualika katika banda lake kuweza kufahamu mengi kuhusu tasnia ya habari nchini Tanzania.
Mbali na hilo utapata nafasi ya kukutana na watangazaji mahiri wa TBC, hasa wale wanaotangaza kwenye Aridhio kama vile Anna Mwasyoke, Anuary Mkama, Elizabeth Mramba, Evance Muhando na wengine wengi.