Afisa ardhi afutwa kazi kwa kusababisha hasara ya bilioni 5

0
385

Afisa Ardhi mkoani wa Arusha, Nikodemus Hilu amefukuzwa kazi kutokana na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 5.

Afisa huyo amesababisha hasara hiyo baada ya kurejesha kwa mwananchi hati ya ardhi ya ekari zaidi ya 3,000 zilizofutwa na Rais John Magufuli, na hivyo mahakama kuamuru serikali kulipa fidia.

Akifungua ofisi ya ardhi ya mkoani Arusha na kukabidhi hati za viwanja kwa wakazi zaidi ya 200, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amehoji sababu ya kurudishwa upya hati ambayo ilifutwa na Rais.

Aidha, Waziri Lukuvi ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza afisa huyo.