TICTS YAKABIDHI VIFAA VYA THAMANI YA MILIONI 182/- KWA WIZARA YA AFYA

0
335

Kampuni ya Upakuaji Mizigo  katika Bandari ya Dar es  Salaam (TICTS) imetoa msaada   wa vifaa  mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi milioni 182, ikiwa ni kuunga  mkono jitihada za Serikali  katika sekta ya afya.


Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada huo  kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Mkurugenzi wa Uendeshaji Donald Talawa amesema kuwa TICTS  ni sehemu  ya watanzania, hivyo inawajibu wa kuunga mkono Serikali katika nyanja mbalimbali.


Talawa amesema kutokana na Serikali kuongeza  vituo vya afya, kampuni hiyo imeona kuna umuhimu wa kusaidia vifaa mbalimbali vitavyosaidia vituo vya afya  kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.


Talawa ametaja vifaa hivyo walivyokabidhi kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni vitanda 100 ,mashuka, mito, vitakasa mikono ambavyo serikali itapeleka katika vituo vya afya.