Polisi afukuzwa kazi kwa kusafirisha dawa za kulevya

0
627

Jeshi la polisi limemfukuza kazi askari wake mwenye namba E 8905 Koplo, Anthony Francis wa Kituo cha Polisi Kisarawe aliyekamatwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi.

Fracis alikutwa akisafirsha dawa hizo kiasi cha kilogramu 76 katika eneo la Nanenane, Manispaa ya Morogoro .

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema askari huyo alikamatwa akiwa amepakia dawa hizo katika gari yake aina ya Toyota Brevis eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro.

Katika tukio jingine, jeshi polisi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kusafirisha milipuko yenye sumu katika basi la kampuni ya Feruzi kinyume cha sheria .

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linaendelea na misako kwa wasafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi ambapo watuhumiwa 22 tayari wanashikiliwa kwa kuhusiaka na biashara hiyo haramu.