Tanzania yazidi kufagiliwa na mataifa mbalimbali

0
307

Norway imeipongeza Tanzania kwa hatua ambazo imezichukua katika kupambana na virusi vya corona kutokana na muongozo wa Rais John Magufuli.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, – Dag-IngeUlstein ametoa pongezi wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Palamagamba Kabudi, mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya video.

Amesema Tanzania ilifanya uamuzi wa maana wa kutoweka zuio kwa wananchi wake kutoka nje kama zilivyofanya nchi nyingi duniani, hali iliyoisaidia kutoathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Waziri Kabudi amemshukuru Waziri huyo wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway kwa kutambua jitihada za Tanzania katika kupambana na virusi vya corona, licha ya baadhi ya nchi kubeza muongozo wa Rais John Magufuli wa kuweka zuio la kutoka nje.

Pia ameishukuru Norway kwa kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kidiplomasia na maendeleo hususani katika kusaidia jitihada za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia malengo yake katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.