Msimu wa mauzo ya tumbaku kuanza karibuni

0
790

Bodi ya Tumbaku Tanzania imetangaza kuanza kwa soko la tumbaku kwa mkoa wa Ruvuma tarehe 22 mwezi huu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo Stanley Mnozya amesema kuwa tumbaku ya msimu huu ina ubora zaidi ya tumbaku ya msimu uliopita kutokana na kubadili matumizi ya mbolea.

Amesema katika msimu huu wa mauzo, halmashauri za mkoa wa Ruvuma zitapata zaidi ya shilingi bilioni moja za ushuru wa zao la tumbaku na wakulima watapata shilingi bilioni 3.4 kutokana na mauzo ya tumbaku.