Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Michael Dunford amempongeza Rais John Magufuli kwa namna alivyoshughulikia kwa ufanisi mlipuko wa virusi vya corona.
Akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Ibuge jijini Dodoma , -Dunford amesema kuwa WFP imefurahishwa na namna Rais Magufuli alivyofikia uamuzi wa kutoweka zuio kwa wananchi wake kutoka nje na kuendelea na shughuli za uzalishaji.
Amesema kuwa hatua hiyo mbali na kuwasaidia Watanzania kuendelea na shughuli za uzalishaji mali, pia iliiwezesha WFP kuendelea na shughuli zake kama kawaida huku ikichukua tahadhari kama ilivyokuwa ikishauriwa na wataalamu wa afya.