Mbatia: Epukeni vyama vyenye siasa za chuki

0
201

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amewataka Watanzania kuwa makini na vyama vya siasa vinavyofanya siasa zenye kujenga chuki kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Akizungumza jijini Arusha na wanachama wa chama hicho kutoka katika wilaya za mkoa huo, Mbatia amewaasa wananchi wachague viongozi wenye kuleta maendeleo na wanaopingana kwa hoja kulingana na sera.