Majina ya sanamu na mitaa kupitiwa upya London

0
618

Meya wa jiji la London nchini Uingereza, – Sadiq Khan amesema sanamu pamoja na majina ya mitaa mbalimbali jijini humo yatapitiwa upya ili kuhakikisha kwamba hayana uhusiano wowote na biashara ya utumwa.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kutokea maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo maarufu kama Black Lives Matter, ambapo waandamanaji waliangusha na kutupa baharini sananu ya mfanyabiashara wa zamani ya utumwa Edward Colston huko Bristol.

Hata hivyo Khan amesema hatarajii sanamu kama ya Churchil kuwa miongoni mwa zile zitakazofanyiwa tathimini.