Marekani: Kifo cha Flyod kubadili mfumo wa utendaji kazi wa polisi

0
786

Idara ya polisi mjini Minnepolis katika Jimbo la Minnesota, Marekani imeahidi kufanya mabadiliko katika idara ya polisi kutokana na kifo cha raia mweusi nchini humo, George Flyod.

Mwenyekiti wa baraza la mji huo, Lisa Bender amesema halmashauri ya jiji imeridhia kuvunjwa kwa idara ya polisi na kuweka muundo mpya wa utendaji kazi wa polisi katika mji huo.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia kifo cha Floyd aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi takribani wiki mbili zilizopita, tukio ambalo limepelekea maandamano ya kitaifa nchini Marekani na katika nchi mbalimbal duniani.

Mwaka jana, afisa mmoja wa polisi wa zamani Mjini Minnepolis alihukumiwa kifungo cha miaka 12 na miezi sita jela kwa kumpiga risasi na kumuua mwanamke mweupe wa Australia ambaye hakuwa na silaha.