Hospitali yashindwa kutoa huduma kwa kukosa umeme na maji

0
470

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula ameliomba Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)  mkoa wa Mwanza pamoja na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA)  kufikisha huduma za umeme na maji katika hospitali mpya ya wilaya Ilemela ili kuiwezesha kuanza kutoa huduma za afya kwa wananchi.


Dkt Mabula ametoa ombi hilo baada ya kukagua majengo ya hospitali hiyo kufuatia taarifa kuwa hospitali hiyo iliyoko eneo la Isanzu manispaa ya Ilemela imeshindwa kutoa huduma, kutokana na kukosekana kwa umeme pamoja na maji.
Ujenzi wa hospitali hiyo mpya ya wilaya ya Ilemela umegharimu shilingi bilioni 1.5 na ni miongoni mwa hospitali 67 nchini zilizojengwa na serikali ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.