Mapato katika sekta ya madini yavunja rekodi

0
355

Serikali imevunja rekodi katika ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya madini, kufuatia kuvuka lengo la kukusanya mapato ya shilingi bilioni 470 kwa mwaka.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amesema makusanyo katika sekta ya madini yamefikia shilingi bilioni 479 na milioni 450 ikiwa bado mwaka wa fedha haujakamilika,
kiwango ambacho ni cha juu zaidi kuwahi kufikiwa.

Amesema siri ya kuongezeka kwa makusanyo hayo ni mabadiliko makubwa yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na serikali katika sekta ya madini.