Zanzibar yaruhusu kuanza shughuli za utalii

0
680

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuanzia hii leo imeruhusu ndege zinazobeba watalii kuwasili visiwani humo, baada ya mambukizi ya virusi vya corona kupungua.

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahmood Thabit Kombo amesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa virusi vya corona si tishio kubwa katika sekta ya utalii.

Hata hivyo Waziri Kombo amesema kuwa pamoja na serikali kuruhusu shughuli za utalii kuendelea, ni vyema shughuli hizo zikaendelea huku tahadhari dhidi ya corona ikiendelea kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na watalii kupimwa pindi wanapoingia visiwani humo.