Netanyahu aanza kujitetea mahakamani

0
364

Waziri Mkuu wa Israel, -Benjamin Netanyahu ameanza kujitetea mahakamani mjini Jerusalem, katika tuhuma zinazomkabili za kuhusika na vitendo vya rushwa pamoja na kutumia madaraka yake vibaya.

Mara kadhaa Netanyahu amekuwa akikanusha kuhusika na tuhuma hizo, na kusema kuwa ni mambo ya kisiasa.

Kwa sasa Netanyahu  anakabiliwa na kesi tatu, ikiwemo ile ya kutuhumiwa kuipendelea kampuni moja iliyofanikiwa sana kibiashara, na ubadhilifu wa mali ya umma.

Kesi zilizokuwa zikimkabili Netanyahu zililazimika kusimama katika kipindi hiki ambacho Taifa hilo likiwa katika njiapanda ya kupata serikali mpya na wakati huohuo likiwa kwenye mapambano dhidi ya virusi vya corona