Zanzibar kulegeza masharti iliyoyaweka kudhibiti corona

0
172

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuregeza masharti iliyoyaweka hapo awali ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
 
Kauli hiyo imetolewa na Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein katika  hotuba yake ya Baraza la Idd El Fitri aliyoitoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, baada ya kukamilika kwa mfungo wa  mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Amesema amri ya kulegezwa kwa masharti hayo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatolewa wakati wowote kuanzia hivi sasa.
 
Machi 19 mwaka  huu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitoa taarifa rasmi kuhusu kuingia kwa virusi vya corona huko Zanzibar na kuweka masharti kumi ili kudhibiti kuenea vya virusi hivyo.
 
Katika hotuba yake Dkt Shein ameelezea kufurahishwa na namna ambavyo wakazi wa Zanzibar walivyoshiriki katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya, jambo  lililochangia kupunguza kiwango cha maambukizi.