Shilingi bilioni 122 zapelekwa HESLB

0
180

Zaidi ya shilingi bilioni 122 zimepelekwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa ajili ya malipo ya wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo Juni Mosi mwaka huu.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amesema hayo jijini Dodoma na kubainisha kuwa kati ya fedha hizo shilingi bilioni 63.7 ni kwa ajili ya malipo ya posho za chakula na malazi.

Dkt Abbasi ameongeza kuwa shilingi bilioni 59 nyingine  ni kwa ajili ya ada kwa Wanafunzi wanaolipiwa na serikali.