Kutokana na changamoto ya uhaba wa walimu wa maabara katika shule nyingi za serikali nchini, wanafunzi wameshauriwa kuyapa kipaumbele masomo ya sayansi ili kuziba pengo hilo.
Hayo yamebainika wakati Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda alipotembelea Shule ya Sekondari Idetemya na kujionea maabara mpya iliyojengwa kwa nguvu za wanachi kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Africa School Association Project (ASAP) .
Aidha, Sweda amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuinua kiwango cha ufaulu na kuondokana na adha ya uhaba wa wanasayansi nchini.
Mratibu wa Africa Project CCorporation, Jackson Zena amesema mradi huo umekamilika na maabara hiyo iko tayari kwa wanafunzi kutumia huku akiwashauri kuchagua mchepuo wa sayansi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Casmir Joseph amewashukuru wadau hao wa elimu na kuwaahidi kuendelea kushirikiana nao kufanya kazi kwa weledi.