Ghasia zaingilia uchaguzi wa Burundi

0
443
Kiongozi wa chama cha upinzani (CNL) nchini Burundi, Agathon Rwasa akiwahutubia wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Ngozi, Aprili 21, 2020. Picha na REUTERS.

Umoja wa Afrika (AU) umeeleza kusikitishwa na ghasia zinazoendelea nchini Burundi katika kipindi hiki ambacho kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu nchini humo zikiendelea.

Katika taarifa yake AU imezitaka pande zote zinazopingana nchini Burundi kusitisha ghasia hizo na kuvitaka vyombo vya ulinzi nchini humo kuhakikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika siku ya jumatano unafanyika katika mazingira huru.

Habari zaidi kutoka nchini Burundi zinaeleza kuwa takribani wanachama mia moja na hamsini wa upande wa upinzani wamekamatwa tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi nchini humo wiki tatu zilizopita.

Rais wa sasa wa Burundi, – Pierre Nkurunziza hagombei kiti cha urais katika uchaguzi ujao, lakini anatarajiwa kuendelea kuwa na nguvu kubwa ya kisiasa.