Mapigano nchini Libya yachukua sura mpya

0
427

Watu kadhaa wamejeruhiwa mjini Tripol nchini Libya, baada ya majeshi yanayomuunga mkono mbabe wa kivita nchini humo Khalifa Hafter kufanya mashambulio katika hospitali moja kwenye mji huo.

Majeshi ya Hafter yameongeza mashambulio dhidi ya serikali ya mpito ya nchi hiyo yenye makao yake makuu mjini Tripol, baada ya jeshi la nchi hiyo kurudisha nyuma majeshi yake yaliyodhamiria kupindua serikali.

Umoja wa Mataifa umesema wananchi wa Libya wanakabiliwa na changamoto kubwa mbili, moja ikiwa ni vita na ya pili ni hatari ya maambukizi ya virusi hatari vya CORONA.

Tayari kuna maambukizi kadhaa ya virusi hivyo nchini humo, huku mashirika ya misaada pia yakishindwa kuwafikishia huduma wahitaji, kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo.

Watu wanaokabiliwa na changamoto kubwa nchini humo ni wahamiaji na wakimbizi kutoka mataifa mengine.