MOSHI: Polisi waagizwa kuwakamata wanaojitangaza kutibu corona

0
214

Diwani wa Kata ya Boma Mbuzi mjini Moshi ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata wale wote wanaojitangaza kuwa wanadawa zinazotibu maambukizi ya virusi vya corona, badala ya kufuata taratibu zinazotakiwa.

Juma Rahibu ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya kutumia kwa ajili ya kujikinga na corona vikiwemo mapima ya kuwekea maji ya kunawa mikono na barakoa.

“Polisi waendelee kuwakata wale wote wanaotangaza dawa za corona ambazo hazijathibitishwa. Hatuwezi leo tukauliwa na corona, halafu kesho tukauliwa na madawa kutoka mitaani,” amesema Rahibu.

Aidha, amewataka wananchi hao wanaotengeneza dawa hizo za asili kufuata taratibu kwa kuziwasilisha katika mamlaka husika kama vile Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Bindamu (NIMR), Wizara ya Afya, Wataalam wa Tiba Asili au Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ili zithibitishwe kama ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Katika kutilia mkazo kwenye hilo amesema hata dawa za corona zilizoagizwa na Rais John Magufuli kutoka Madagascar hivi karibuni hazijaanza kutumiwa hadi zitakapothibitika kuwa ni salama, hivyo ni vyema na wananchi wakaiga mfano huo.

Wakati huo huo, amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua wale wote wanaotoa taarifa za upotoshaji kuhusu ugonjwa wa corona ikiwemo idadi ya vifo na wale wanaosema kila kifo hata cha malaria au presha wanasema ni sababu ya corona