Serikali kuamua hatma ya Ligi Kuu Tanzania

0
462

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limesema hatma ya kurudi kwa mashindano yake yote kunategemeana na maamuzi ya serikali juu ya mlipuko wa virusi vya corona.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho inaeleza kuwa kwa sasa wanaendelea na michakato ya ndani kuhusu kurejea kwa ligi mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Jumapili, Mei 4 mwaka huu, Rais Dkt. John Magufuli alisema atakaa na watalaamu wake ili kuweza kuangalia uwezekano wa kuirejesha michuano ya soka hapa nchini.

Michezo yote na shughuli mbalimbali zinazohusisha mikusanyiko ya watu zilizuiwa tangu katikati mwa mwezi Machi 2020, ikiwa ni sehemu ya hatua zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na maambukizi ya homa ya mapafu (COVID-19).