Kiongozi wa Korea Kaskazini ajitokeza baada ya kuzushiwa ugonjwa

0
698

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu cha ukimya, huku kukiwa na uvumi kwamba huenda kiongozi huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo.

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Utangazaji la Korea Kaskazini (KCNA) zimemuonesha kiongozi huyo akikata utepe kuzindua kiwanda cha mbolea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).

Kim hakuonekana hadharani tangu Aprili 12 alipozungumza na wananchi katika hotuba ya kitaifa iliyorushwa na vyombo vya habari.