Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga unatarajiwa kuzikwa leo huko Tosamaganga mkoani Iringa.
Mazishi hayo, mbali na kuhudhuriwa na viongozi wengine, yataongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu.
Dkt. Mahiga ambaye alijizolea umaarufu kutokana na uadilifu na uongozi wake alifariki dunia Mei 1, 2020 baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake jijini Dodoma.
Hapa chini ni wasifu mfupi wa kiongozi huyo;