Nchi mbalimbali Duniani zaendelea kuchukua tahadhari ya COVID-19 huku nyengine zikilegeza masharti

0
550

Ujerumani imeamuru matumizi ya lazima ya barakoa kwa wananchi wake ambapo wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imeagiza shehena kubwa ya barakoa kutoka nchini China

Uamuzi huo wa Ujerumani ni hatua zaidi katika kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Homa Kali ya Mapafu – Covid-19.

Wakati hayo yakiendelea Umoja wa Mataifa umeonya kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kurudisha nyuma juhudi za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo ambapo mataifa mbalimbali duniani yameendelea kutangaza kulegeza masharti ya kuzuia watu kutoka nje ikiwa ni hatua ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mataifa yaliyotangaza nia ya kulegeza masharti ya kuzuia watu kutoka nje ni pamoja na Marekani, China, India, Australia, New Zealand, Italia, Hispania, Ubelgiji na Iran.