Wafanyabiashara watakiwa kutopandisha bei za bidhaa Mwezi wa Ramadhan

0
590

Waumini wa dini ya kiislamu nchini leo wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo waumini hao hufunga kwa siku 29 au 30 kutegemea na kuandama kwa mwezi

Viongozi mbalimbali nchini akiwemo Rais Dkt John Magufuli Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wamewatakia waislamu kote nchini mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku wakiwataka wananchi kuendelea kuliombea Taifa ili liepukane na ugonjwa wa COVID-19

Kwa upande wake katibu wa Baraza la Ulamaa la Baraza kuu la Waislamu Tanzania – BAKWATA Shekhe Hassan Chizenga amesema Baraza hilo litatoa mwongozo wa elimu ya kinga unaozingatia mtazamo wa dini na ushauri wa wataalamu wa Afya dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

Aidha wafanyabiashara wameaswa kutotumia vibaya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kupandisha bei za vyakula hasa vile ambavyo hutumika kwa futari