Wagonjwa wa corona wafikia 147

0
594

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametangaza kuongezeka kwa wagonjwa wapya 53 wenye maambukizi ya virusi vya corona na kupelekea jumla ya visa vya Corona kuwa 147.

Waziri Ummy Ametaja mikoa iliyokutwa na visa vipya vya Corona ni:

38 – Dar es Salaam
10 – Zanzibar
1 – Kilimanjaro
1 – Mwanza
1 – Lindi
1 – Kagera
1 – Pwani

Wizara inaendelea kuwasisitiza wananchi kujikinga na virusi hivyo kwa kufuata taratibu zinazotolewa ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuepuka misongamano pamoja na kuahirisha safari zisizo na lazima.