Elimu ya corona kuanza kutolewa mitaani

0
555

Serikali imezindua mpango maalumu wa kutoa elimu ya afya kwa umma katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kuwapo kwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona, ikiwa ni mwendelezo wa kuwafikia watu wengi katika ngazi ya mtaa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizundua mpango wa elimu ya afya kwa umma kwa siku 20 ambao utaongozwa na vikundi vya kijamii kwa kushirikiana na Msalaba Mwekundu chini ya wizara ya afya.

Waziri Ummy amesema lengo la kuzindua mpango huo ni kukata mnyororo wa maambukizi ya corona kati ya mtu na mtu kwa kutumia vikundi vya kijamii ambavyo vitaelimisha na kutoa taarifa sahihi kwa jamii kuhusu ugonjwa wa homa ya mapafu.

Katika mpango huo magari 18 yatatumika kwa siku 20 na yatakwenda katika maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile masoko, stendi.