Visa vya waathirika corona Kenya vyafikia 208

0
918

Serikali ya Kenya imetangaza ingezeko la visa vipya 11 vya maambukizi ya virusi vya corona, hivyo kufanya idadi ya waathirika kufikia 208.

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema visa hivyo vimetokana na sampuli 674 zilizopimwa ndani ya saa 24 zilizopita, na waathirika wana umri kati ya mwaka 1 hadi miaka 42.

Waathirika wote 11 ni raia wa Kenya, ambapo wanne kati ya wana historia ya kusafiri Falme za Kiarabu na walikuwa wamewekwa karantini.

Aidha, Kagwe amesema kuwa watu 14 wameruhusiwa kurejea makwao baada ya kupona ugonjwa wa homa ya mapafu, hatua iliyopelekea watu waliopona kufikia 40.

Pia, waziri huyo amethibitisha kifo cha mgonjwa mmoja hivyo kupeleka watu waliofariki tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa kufikia 9.