Waziri wa afya ataka watoto na wazee walindwe

0
869

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amewataka Watanzania kuendelea kuzingatia kanuni za afya zinazotolewa na wataalamu ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, wakati wakisherehekea sikukuu ya pasaka.

Ummy Mwalimu ameyabainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakati akitoa salamu za Pasaka kwa Watanzania, huku akiwasisitiza kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, na kuwalinda zaidi wazee na watoto.

“Heri ya Pasaka, baki salama, Corona inazuilika. Epuka mikusanyiko. Tuwalinde watoto na wazee,” ameandika Waziri Ummy.

Hadi Aprili 11, 2020, Tanzania imerekodi visa 32 ambapo kati ya watu watano wamepona, watu watatu wamefariki, huku waliobaki wakiendelea vizuri na matibabu.