Serikali yaamuru mshindi wa BSS 2019 alipwe

0
1356

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production chini ya Mkurugenzi wake Madam Ritta Paulsen inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki (Bongo Star Search-BSS) kuhakikisha wamemlipa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ya mwaka 2019 kama walivyoahidi kutoa zawadi kiasi cha shilingi milioni 50.

Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kueleza umma jitihada ambazo serikali imefanya baada ya kupokea barua ya malalamiko ya kuto kulipwa kwa mshindi huyo kutoka kwa familia yao.

Kwa upande wa mshindi huyo, Meshack Fukuta amesema mpaka sasa kampuni hiyo imemlipa kiasi cha shilingi milioni moja tu na siyo milioni mbili kama wanavyosema.

Pamoja na hayo Shonza amewasisitiza wasanii kuhakikisha wanaandikishiana mikataba na watu mbalimbali wanaofanya nao kazi.

Mashindano hayo BSS yalifanyika Desemba 24, 2019 Jijini Dar es Salaam.