Mratibu wa mshindano ya mpira wa kikapu ya vijana ya NBA Junior, Bahati Mgunda amesema hakuna tatizo kwa mashindano hayo kufanyika nje ya jiji la Dar es Salaam kama wahusika watafuata taratibu zinazohitajika.
Akiongea na TBC, Mgunda anasema ili mikoa mingine iweze kupata nafasi ya kuandaa mashindano hayo inabidi iwasiliane na NBA ambao ndio wahusika wakuu wa mashindano hayo.
Mashindano ya Junior NBA, yanafanyika kwa ushirikiano mkubwa na NBA ya Marekani kwa lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia mchezo wa mpira wa kikapu na mpaka sasa tayari mamia ya vijana wamenufaika na mpango huo.