Wakulima wadogo wa choroko wilayani Magu mkoani Mwanza wameiomba serikali kuwaruhusu kuuza choroko zao kwa mnunuzi anayewalipa fedha taslimu badala ya kupeleka katika Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) kwa kuwa havina fedha
Kauli hizo za wakulima wadogo zimekuja kufuatia serikali wilayani Magu kupiga marufuku wafanyabiashara kununua choroko kutoka kwa wakulima baada ya malori matatu yaliyokuwa na zaidi ya tani 50 za choroko kukamatwa na kutaifishwa kwa madai kuwa zilinunuliwa kutoka kwa wakulima badala ya kutoka AMCOS.
Diwani wa Kata ya Kabila, Edward Kihamba ameishauri serikali kuwaruhusu wafanyabiashara kuuza choroko walizonunua kabla ya tangazo la serikali la Februari 14.
Wanunuzi wa choroko wamesema hununua kilo moja ya choroko kwa bei ya kati ya shilingi 1,250 hadi 1,300 ambayo wakati mwingine ni zaidi ya hata ile ya AMCOS.