Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte afariki dunia

0
279

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte amefariki duniani leo Machi 30, 2020

Shamte amefariki dunia akiwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya Msemaji wa MOI Patrick Mvungi inaeleza kuwa Kiongozi huyo aliwasili hospitalini hapo Machi 23 mwaka huu akitokea Gereza la Maweni Tanga ambapo alikuwa ameshikiliwa kwa tuhuma za uhujumu uchumi zinazojumuisha kosa la utakatishaji fedha.

Kutoka kwa familia, Mariam Shamte amesema kuwa mume wake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo, na kwamba amefanyiwa upasuaji mara kwa mara.

Hivi karibuni Shamte aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kutokana na kuwa Mwenyekiti wa TPSF.