Wananchi wa Mali leo wanapiga kura kuchagua wabunge wa nchi hiyo huku kukiwa na wasiwasi wa usalama wa afya kwa raia wa nchi hiyo kutokana na janga la virusi vya Corona.
Hapo jana nchi hiyo ilitangaza kifo cha kwanza kutokana na virusi hivyo.
Vyama kadhaa vya upinzani vilitoa wito wa kuahirishwa uchaguzi huo kutokana na janga la COVID-19, ambapo watu 18 wameambukizwa nchini humo tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa wiki hii.
Kutekwa nyara kwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Soumaila Cisse mapema wiki hii pia kinaelezwa kuweka dosari ya zoezi hilo.
Habari zinaeleza kuwa Cisse huenda yuko mikononi mwa kundi la wanamgambo wa itikadi kali.
Uchaguzi huo wa wabunge umekuwa ukihairishwa mara kwa mara tangu mwaka 2018 kuhofia usalama wa raia kutokana na mashambulio nchini humo yanayotekelezwa na makundi ya kigaidi.