Mwanasoka Nouri azinduka baada kupoteza fahamu kwa miezi 33

0
1472

Kiungo wa timu ya Ajax ya nchini Uholanzi, Abdelhak Nouri aliyeanguka na kupoteza fahamu uwanjani mwezi Julai mwaka 2017, amezinduka.

Nouri mwenye umri wa miaka 22, alianguka na kupoteza fahamu baada ya kupata shambulio la moyo katika mchezo wa kirafiki kati ya timu yake ya Ajax na Werder Bremen.

Kwa mujibu wa kaka yake, Nouri baada ya kuwa kwenye hali ya kutojitambua kwa muda wa miaka miwili na miezi tisa, amezinduka na fahamu kumrejea na sasa ana uwezo wa kuchezesha macho na kula kwa njia ya kawaida.