Mahakama Zanzibar zasitisha kazi kwa siku 30

0
240

Mahakamu Kuu Zanzibar imesitisha zoezi la kusikiliza kesi kwa kipindi cha mwenzi mmoja kuanzia leo Machi 26 hadi Aprili 24 mwaka huu ikiwa utekelezaji wa agizo la serikali la kuondoa misongamano ya watu ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar, Mohamed Ali Mohamed amesema mahakama itashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana huku muombaji na wakili pekee ndio watakao ruhusiwa kuingia mahakamani.

Aidha, Mohamed amesema licha ya kuwa usikilizwaji wa kesi umesitishwa, watendaji wa mahakama wataendelea kubaki katika maeneo yao ya kazi.