Mawaziri wa afya Afrika Mashariki kufanya mkutano wa dharura

0
523

Mawaziri wa afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajia kufanya mkutano leo kwa ajili ya kuweka mikakati ya pamoja wa kutokomeza virusi vya Corona.

Mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya video utaangazia njia zaidi za kudhibiti maambukizi mapya ya virusi hivyo ambavyo vimewakumba watu 73 katika nchi za Tanzania, Uganda, Kenya na Rwanda, huku kukiwa hakuna muathirika aliyeripotiwa nchini Sudan Kusini na Burundi.

Njia mbalimbali ambazo zimetumiwa mapaka sasa na nchi hizo kudhibiti virusi hivyo vinavyosababishwa homa ya mapafu ni pamoja na kufunga shule, vyuo na taasisi nyingine za mafunzo, kufunga mipaka pamoja anga, kuzuia mikusanyiko ya watu.

Taarifa iliyotolewa na EAC imeeleza kuwa sekretarieti ipo katika mchakato wa kugawa maabara zinazotembea (mobile laboratories) pamoja na vipimo vya COVID-19 kwa nchi wanachama wote.

Kila nchi mwanachama itapatiwa magari manne (4WD) yenye maabara na vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo zina uwezo wa kupima Ebola la COVID-19.