TRC yafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali iliyoua wafanyakazi watano

0
227

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali iliyohusishwa na treni ya uokoaji na kiberenge na kupelekea vifo vya wafanyakazi watano wa shirika hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Masanja Kadogosa amesema kuwa, ajali hiyo imetokea katika eneo la katikati ya stesheni za Mwakinyumbi na Gendagenda mkoani Tanga ambapo wafanyakazi wanne walifariki dunia papo hapo na mwingine alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe (Magugu).

Mtu mmoja aliyejeruhiwa katika ajali hiyo anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Magugu.