Mwana FA ajitangaza kuwa ni miongoni mwa wagonjwa sita wa corona

0
1805

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, amejitangaza kuwa yeye ni miongoni mwa wagonjwa sita waliothibitika kuwa na homa ya corona nchini.

Kupitia video aliyoisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Mwana FA amesema hivi karibuni alirejea nchini kutoka nchini Afrika Kusini na kuanza kusikia homa kali, na baada ya kuchukuliwa vipimo vimeonyesha kuwa na homa ya corona.

Amesema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na kwamba tangu aliporejea nchini kutoka Afrika Kusini amejitenga na watu ili kuepuka kuwaambukiza.

Mwana FA amesisitiza watu kuendelea kujilinda na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ili kuepuka maambukizi.