Meneja wa Diamond akutwa na Corona

0
1916

Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK amethibitisha kuwa ana maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19), lakini ameeleza kuwa afya yake inaendelea vizuri.

Sallam kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa yupo chini ya uangalizi na huduma anazopatiwa ni nzuri.

“… nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na Coronavirus, kwa sasa nipo chini ya uwangalizi mzuri na afya yangu inaendelea vizuri,” ameandika Sallam.

Aidha, ameishukuru serikali kwa namna inavyoshughulikia waathirika wa ugonjwa wa COVID-19, na pia amewataka Watanzania kufuata ushauri wa wizara ya afya ili kuweza kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.

“…hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye wizara husika, naomba kwa wote tuwe salama na familia zetu, tuchukue tahadhari mapema,” amehitimisha Sallam.