Idadi ya wagonjwa wa Corona yaongezeka nchini

0
570

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza kufungwa kwa vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini kuanzia leo, kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kufanya mabadiliko kwenye mihula ya masomo ili kuwawezesha hata wale waliokaribia kufanya mitihani wapate muda wa kufanya mitihani yao katika siku za baadae.

Akitoa taarifa kwa wananchi kuhusu virusi vya corona, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa wagonjwa wengine wawili ya corona wamethibitika kuwepo nchini ambao mmoja ni raia wa Marekani aliyepo jijini Dar es salaam na mwingine raia wa Ujerumani aliyepo Zanzibar.

Kugundulika kwa wagonjwa hao wawili kunaifanya Tanzania kuwa na wagonjwa watatu wa homa ya corona.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu ameendelea kuwasihi Watanzania wote kutokua na hofu dhidi ya virusi hivyo, kwa kuwa serikali inafanya jitihada kubwa kuhakikisha havienei.