Polisi yakamata wapiga ramli chonganishi

0
186

Watu 216 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kujihusisha na ramli chonganishini, wizi wa mifugo, imani za kishirikina, wivu wa mapenzi, pamoja na vitendo vya kulipa visasi.

Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Mihayo Msekela ametoa taarifa hiyo katika bwalo la polisi mkoani Geita na kueleza kuwa operesheni hiyo ya pili imefanyika katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Kagera, Simiyu, Tabora, na Mwanza.

Ameongeza kuwa katika operesheni ya kwanza iliyofanyika Februari 15 mwaka huu jumla ya watuhumiwa 504 walikamatwa wakituhumiwa kutenda makosa mbalimbali, na kwamba sasa idadi ya watuhumiwa wote ni 720.

Wakati huo huo, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, Kamanda Msekela amewatunuku vyeti vya pongezi askari 15 wa jeshi hilo mkoani Geita kutokana na utendaji wao uliotukuka katika majukumu yao.