Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Janeth Mghamba amesema kuwa pamoja na majibu ya sampuli za mtandao wa watu waliokutana na mgonjwa wa homa ya corona aliyegundulika mkoani Arusha kuonyesha kuwa wako salama, bado wataendelea kuwachunguza watu hao kwa muda siku 14.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Dkt Mghamba amesema kuwa wamejiridhisha na majibu hayo kutokana na uhakika wa maabara iliyopo nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha, -Mrisho Gambo amesema kuwa wakazi wengi wa mkoa huo walipata hofu kuhusu washukiwa hao lakini majibu yamejidhihirisha kuwa wako salama na kinachotakiwa ni wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.