TBC kuboresha usikivu katika wilaya 15

0
115

Katika kipindi cha mwaka huu, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) litaendelea kuboresha usikivu wa matangazo yake katika wilaya kumi na tano nchini.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza wakati akifungua mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo.
Amesema kuwa, iwapo usikivu wa matangazo ya TBC utaboreshwa katika wilaya hizo kumi tano, usikivu huo utakua umeboreshwa kwenye wilaya zaidi ya mia moja katika uongozi wa serikali ya awamu ya tano.
Naibu Waziri Shonza ameongeza kuwa, maboresho ambayo yamekua yakifanyika ndani ya Shirika hilo yamewafanya Wananchi wengi kuendelea kuamini TBC kama chanzo chao muhimu cha kupata habari.