Wafanyabiashara Soko la Madini Dar es Salaam wapaza sauti

0
222

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewaahidi wafanyakazi katika Soko la Madini la Dar es Salaam kutatua changamoto walizonazo ikiwa ni pamoja na kuondoa leseni za masonara.

Nyongo amesema hayo baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa soko hilo katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Dunstan Kitandula amesema kwamba, kwa sasa hali ya soko hilo inaendelea vizuri na kwamba tangu kuanzishwa kwake Julai 2019 kumesaidia kuondoa matapeli waliokuwa wakiuza bidhaa bandia.

Katika kipindi cha miezi saba hadi kufikia Februari 2020 Soko la Madini la Dar es Salaam limefanikiwa kuuza vito vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.9 na dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 5.1.