Corona yatishia mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA

0
235

Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (UMISETA) na Umoja wa Michezo Shule za Msingi (UMITASHUMTA) yamesitishwa kutokana na mlipuko wa homa ya Corona.

Amesema hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Mbali na Wizara ya Afya kuthibitisha kutokuwepo kwa mgonjwa wa Corona nchini hadi hivi sasa, Jafo amesema ni vyema tahadhari zikachukuliwa kijikinga na homa hiyo.

Aidha, Jafo ameomba uongozi wa shule za juu kufanya mahafali bila wageni.

“Kuhusu mahafali ya kidato cha sita, hatujakataza kufanyika tunachosema kama kuna haja ya kufanya mahafali hayo basi shule zinazofanya zisihusishe wageni kutoka nje ya shule badala yake wafanye walimu, wanafunzi, na watumishi wa shule husika,” amesema Jafo.

Mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA huhusisha shule kutoka mikoa mbalimbali nchini.