Rais Magufuli asitisha mbio za Mwenge

0
466

Rais John Magufuli ametangaza kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu, zilizotarajiwa kuanza Aprili 2 huko Unguja, kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Coronaa.

Amesema kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zitapelekwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kuimarisha huduma za kinga dhidi ya corona.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela (Ubungo Interchange).

Mradi wa ujenzi huo umefikia asilimia 70 na hadi utakapokamilika utakua umegharimu shilingi bilioni 230.