Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC)- Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole asubuhi hii amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kumlipia faini ya shilingi milioni 30 Dkt. Vicent Mashinji, aliyekua Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye baadae alihamia CCM.
Hapo jana Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba aliwahukumu viongozi waandamizi wa CHADEMA pamoja na Dkt. Mashinji kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 350 au kifungo cha miezi mitano jela kwa kila kosa, baada ya kuwakuta na hatia katika makosa 12.
Katika mgawanyo wa faini hiyo, Dkt. Mashinji anatakiwa kulipa shilingi milioni 30.